London,England.
Mshambuliaji wa klabu ya Chelsea Patrick Bamford amevunja mkataba wake wa mkopo katika klabu ya
Crystal Palace na kuamua kurejea Stamford Blidge baada ya kuchoka kukaa benchi.
Bamford,22 amefikia uamuzi huo baada ya kufanikiwa kucheza michezo sita tu msimu huu tena yote akiingia kutokea benchi huku jumla ya dakika alizocheza zikiwa ni 119.
Wakati huo Bamford amesema yuko tayari kuhamia klabu nyingine kwa mkopo baada ya ripoti kudai kuwa Norwich na Bournemouth zinaitaka huduma.
0 comments:
Post a Comment