Dar es salaam,Tanzania.
Klabu ya Azam FC imeendelea kuipumulia Yanga kileleni mwa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya jioni ya leo kuilaza Kagera Sugar kwa mabao 2-0 katika mchezo mkali uliopigwa katika dimba la Azam Complex,Chamazi jijini Dar es salaam.
Mabao yaliyoipa ushindi Azam FC yametiwa kimiani dakika za 9 na 74 na mshambuliaji Kipre Tchetche kwa kichwa na mlinzi Shomari Kapombe huku Salum Kanoni akishindwa kuifungia bao la kufutia machozi Kagera Sugar baada ya mkwaju wake wa penati kuokolewa na mlinza mlango Aishi Manula.
Kufuatia ushindi huyo Azam FC imefikisha pointi 32 baada ya kucheza mechi 12,ikizidiwa pointi moja na
Yanga yenye pointi 33 baada ya kucheza michezo 13.
Katika mchezo mwingine wa ligi kuu Toto Africans imeshindwa kuutumia vyema uwanja wake wa nyumbani wa CCM Kirumba baada ya kufungwa bao 1-0 na African Sports ya Tanga.
0 comments:
Post a Comment