LONDON
Klabu ya Chelsea imemteua kwa mara nyingine tena Muholanzi Guus Hiddink kuwa kocha wake wa muda kuziba nafasi ya Jose Mourinho aliyetimuliwa kazi siku ya alhamis kufuatia muendelezo wa matokeo mabaya.
Hiddink,69 aliyekuwa jukwaani wakati Chelsea ikiitandika Sunderland mabao 3-1 jana jumamosi ataifundisha klabu hiyo mpaka mwisho wa msimu wakati uongozi ukifanya mipango ya kumpata kocha wa kudumu.
Hii ni mara ya pili kwa Hiddink kujiunga na Chelsea kama kocha wa muda,;mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka 2009 baada ya Mbrazil Louis Felipe Scolari kufutwa kazi na kufanikiwa kuiongoza Chelsea kutwaa kombe la FA pamoja na kufika nusu fainali ya ligi ya mabingwa.
Akifanya mahojiano baada ya uteuzi huo Hiddink amesema anafuraha kujerea kwa mara nyingine Stamford blidge na ana imani atapata ushirikiano mkubwa toka kwa wachezaji,mashabiki na wafanyakazi wenzake na kuongeza kuwa Chelsea ni klabu kubwa na haipaswi kuwa hapo ilipo sasa hivyo atafanya kila aliwezalo kuhakikisha Chelsea inafanya vizuri.
Hiddink anatarajiwa kukianza kibarua chake wakati Chelsea itakapovaana na Watford Desemba 26 kisha Manchester United Desemba 28.
Kabla ya kujiunga na Chelsea Hiddink amewahi kuvifundisha vilabu vya PSV Eindhoven,Fenerbahce, Valencia,Real Madrid, Real Betis na Anzhi Makhachkala.Pia amewahi kuzifundisha timu za taifa za Netherlands, South Korea, Australia, Russia na Uturuki.
0 comments:
Post a Comment