Liverpool,England.
Liverpool imeshindwa kutamba nyumbani baada ya kulazimishwa sare ya magoli 2-2 na West Bromwich Albion katika mchezo maridadi wa ligi kuu nchini England uliopigwa katika dimba la Anfield.
Liverpool ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa nahodha wake Jordan Henderson aliyefunga dakika ya 22.Kuingia kwa bao hilo kuliiamsha West Bromwich Albion ambayo ilikuja juu na kufanikiwa kupata mabao mawili kupitia kwa Craig Dawson dakika ya 30 na Jonas Olsson dakika ya 74 kabla ya Divok Origi kuisawazishia Liverpool dakika ya 90 na kuinusuru na aibu nyumbani.
Katika mchezo mwingine uliopigwa huko White Hart Lane Newcastle United imeifunga Tottenham kwa jumla ya mabao 2-1.
Magoli yaliyoipa ushindi Newcastle United yamefungwa na Alexander Mitrovic dakika ya 74 na Ayoze Perez dakika ya 90 huku lile la kujifariji la Tottenham likifungwa na Erik Dier dakika ya 39.
0 comments:
Post a Comment