Mendez na Mourinho
Manchester, England.
Wakala wa kocha Jose Mourinho Mreno Jorge Mendez amesema habari zilizoenea kuwa mteja wake ameshafikia makubaliano ya kuifundisha Manchester United ni uzushi mtupu na hazipaswi kuaminiwa kabisa.
Mendez akifanya mahojiano ya Globo Esporte amesema hakuna kitu kama hicho na kwasasa yeye na mteja wake [Mourinho] hawajui kitakachotekea siku za usoni na amesisitiza kuwa hakuna makubaliano yoyote yaliyofikiwa ama ofa yoyote iliyoletwa mezani kujadiliwa.Hii siyo kweli.
Kauli hiyo ya Mendez imekuja baada ya jana jumanne habari kuenea kuwa Mourinho ameshafikia makubaliano na Manchester United ili kuziba nafasi ya Louis Van Gaal ambaye muda wowote atatupiwa virago.
0 comments:
Post a Comment