728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, December 22, 2015

    ABRAMOVIC HATAKI GUARDIOLA AENDE MAN CITY,AJA NA STAILI YA KIFISADI ZAIDI



    LONDON,ENGLAND.

    Mmiliki wa Chelsea Mrusi ROMAN ABRAMOVIC hataki kuona Pep Guardiola akienda Manchester City na badala yake ametamba kuwa atafanya kila awezalo kuhakikisha kocha huyo Muhispania anatua katika klabu yake tena kwa gharama yoyote ile.

    Taarifa kutoka nchini England zinadai kuwa Abramovic anataka kumshawishi Guardiola asiende Manchester City kwa kumlipa kiasi chochote kile cha pesa atakachokitaka pamoja na kumpa pesa nyingi ya kufanyia usajili ikiwezekana hata kukibadili kabisa kikosi kizima cha Chelsea ambacho msimu huu kimeboronga vilivyo ligi kuu.

    Sababu nyingine inayoipa Chelsea kiburi kuwa itafanikiwa kumnasa Guardiola ni kuwa mke wa kocha huyo aitwaye Cristina Serra anavutiwa zaidi na maisha ya jiji la London iliko Chelsea kuliko jiji la Manchester viliko vilabu vya Manchester City na Manchester United.




    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: ABRAMOVIC HATAKI GUARDIOLA AENDE MAN CITY,AJA NA STAILI YA KIFISADI ZAIDI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top