728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, December 25, 2015

    GIROUD AJIVUNIA SOKA LA MCHANGANI


    London,England.

    Mshambuliaji wa Arsenal aliye katika kiwango bora kwa sasa Olivier Giroud amesema kuanzia soka lake katika ligi za madaraja ya chini huko nyumbani kwao Ufaransa ndiko kuliko mfanya awe mchezaji imara,mkakamavu na mvumilivu kuliko wachezaji waliopitia katika shule za soka [Akademi].

    Giroud,29 ambaye kabla ya kujiunga na Arsenal mwaka 2012 akitokea Montpellier alinza soka lake kwa kucheza madaraja ya tatu na pili akiwa na vilabu vya Grenoble, Istres na Tours anaamini mafanikio aliyonayo sasa yanatokana na changamoto [magumu] alizokutana nazo enzi zile anacheza ligi za mchangani.

    Giround ambaye ameifungia Arsenal magoli sita katika michezo minne ya hivi karibuni ameongeza kuwa asingekuwa imara kama angepitia katika shule maarufu za soka za vilabu kama Marseille, PSG ama Lyon kwani wachezaji wanaotoka hapo huwa ni kama huwa ni laini laini.

     




    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: GIROUD AJIVUNIA SOKA LA MCHANGANI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top