KLABU BINGWA YA DUNIA:BARCA BILA MESSI YAWACHAPA WACHINA TATU MTUNGI NA KUTINGA FAINALI
Yokohama,Japan.
Klabu ya FC Barcelona imetinga fainali ya michuano kombe la vilabu bingwa duniani baada ya leo mchana kuifunga klabu ya Guangzhou
Evergrande ya China kwa mabao 3-0 katika mchezo wa nusu fainali uliopigwa katika dimba la Yokohama.
FC Barcelona ambayo leo haikuwa na nyota wake Lionel Messi anayesumbuliwa na maumivu ya tumbo imepata mabao yake dakika za 39' 50' 67' kupitia kwa mshambuliaji wake Louis Suarez.
0 comments:
Post a Comment