Elche,Hispania.
Klabu ya Elche imeamua kuiburuza mahakamani ligi ya La Liga (LFP) na kutaka ilipwe zaidi ya euro milioni 60 kama fidia baada ya kushushwa daraja kibabe msimu uliopita.
Kutoka AS na Onda Cero taarifa zinasema kuwa Elche imeamua kwenda mahakamani kudai pesa hiyo itakanayo na haki za matangazo ya televisheni kwa madai kuwa ilikuwa ni haki yao kama wasingeshushwa daraja kibabe dai ambalo limeendelea kupingwa vikali na LFP.Huku pia ikisisitiza pesa hiyo ni pamoja na fidia ya kukimbiwa na nyota wake baada ya klabu kushushwa daraja.
Elche ilishushwa daraja msimu uliopita baada ya kukumbwa na tatizo la kiuchumi pamoja na madeni makubwa ya kodi lakini uongozi wa klabu hiyo ukiongizwa na Juan Serrano umesisitiza kuwa Elche ilikidhi vigezo vya kubaki La Liga baada ya kumaliza ligi ikiwa katika nafasi ya 13.
KAULI YA LA LIGA
La Liga imepinga kuishusha kibabe Elche na kudai klabu hiyo ilishindwa kuwasilisha kwa wakati nyaraka zote muhimu za utetezi na kuamua kuishusha mpaka ligi daraja la pili (Segunda) na nafasi yake kupewa klabu ya Eibar iliyokuwa tayari imeshaiaga ligi ya La Liga.
0 comments:
Post a Comment