728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, December 22, 2015

    GOR MAHIA YACHOMOA KUSHIRIKI MAPINDUZI CUP


    Nairobi,Kenya.

    Mabingwa wa ligi kuu ya Kenya (KPL) Gor Mahia wamechomoa kushiriki michuano ya Mapinduzi Cup inayotarajiwa kutimua vumbi lake Januari mwakani huko Zanzibar kwa madai kuwa wana ratiba ngumu mwanzoni katika kipindi hicho.

    Uamuzi huo wa Gor Mahia umefikiwa leo baada ya kikao cha kamati kuu ya klabu hiyo ikiongozwa na mwenyekiti wake Ambrose Rachier kuutupilia mbali mwaliko huo kutoka ZFA na badala yake kamati hiyo imeipa baraka Gor Mahia kushiriki michuano maalumu ya kuadhimisha miaka 80 tangu kuanzishwa kwa klabu ya St.George.

    Michuano hiyo inayoitwa St George 80th anniversary inatarajiwa kuanza kutimua vumbi lake huko Addis Ababa,Ethiopia Januari 10 mwakani na kuisha Januari 14 na itashirikisha vilabu vinne ambavyo ni wenyeji St George,Gor Mahia, El Merreikh na Saint Michael United.

    Aidha baada ya michuano hiyo Gor Mahia pia itashiriki michuano mingine iitwayo Fidel Odinga Memorial Cup.Michuano hiyo ni maalumu kwa ajili ya kumkumbuka shabiki maarufu wa klabu hiyo Fidel Odinga [Mtoto wa waziri mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga] aliyeuwawa mwaka jana.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: GOR MAHIA YACHOMOA KUSHIRIKI MAPINDUZI CUP Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top