Lagos,Nigeria.
Mshambuliaji mahiri wa Watford ya Odion Ighalo anahitaji magoli 3 tu ili aweze kuifikia rekodi iliyowekwa na Mnigeria mwenzake Yakubu Aiyegbeni ya kufunga magoli 16 katika msimu mmoja wa ligi kuu nchini England.
Ighalo,24 ambaye juzi jumamosi aliifungia Watford goli moja katika mchezo ulioisha kwa sare ya 2-2 dhidi ya Chelsea katika dimba la Stamford Bridge ameapa kufanya kila awezalo kuhakikisha anafunga magoli mengi ambayo yatamng'arisha yeye pamoja na klabu yake ya Watford iliyoko katika nafasi ya saba ikiwa na pointi zake 29 baada ya kushuka dimbani mara 18.
Yakubu Aiyegbeni ndiye anayeshikilia rekodi ya kuwa Mnigeria aliyefunga magoli mengi zaidi katika ligi kuu ya England tangu ilipoasisiwa mwaka 1992 baada ya msimu wa mwaka 2003/04 kuifungia Portsmouth magoli 16.
Nafasi ya pili inashikiliwa na Peter Odemwingie mwenye magoli 15 aliyoyafunga akiwa na West Bromwich Albion msimu wa mwaka 2010/2011 huku Ighalo akifuatia katika nafasi ya tatu baada ya kufanikiwa kuifungia Watford magoli 13 msimu huu.
Ighalo huenda akaendeleza tena moto wake wa kupachika magoli jumatatu hii wakati atakapoiongoza Watford kuivaa Tottenham
Hotspur katika dimba lake la nyumbani la Vicarage Road.
0 comments:
Post a Comment