Liverpool,England.
Klabu ya Liverpool imeshinda mbio za kumnasa kiungo wa Red Star Belgrade Marco Grujic baada ya ofa yake ya paundi millioni 5 kukubaliwa na miamba hiyo ya Serbian Super Liga.
Grujic,19 ambaye kiuchezaji anafananishwa na kiungo wa Chelsea Nemanja Matic anatarajiwa kutua Merseyside wiki hii kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya na ikiwa atafuzu atasaini mkataba wa miaka mitano kuichezea Liverpool.
Hata hiyo Grujic aliyekuwa pia akimezewa mate na vilabu vya Chelsea,Udinese,Sassuolo na Inter Milan hataweza kuichezea Liverpool msimu huu kwani tayari kuna makubaliano kuwa atakopeshwa Red Star Belgrade mpaka mwisho wa msimu kwa ada ya euro millioni 1.
0 comments:
Post a Comment