728x90 AdSpace

Sunday, December 13, 2015

KOMBE LA DUNIA LA VILABU:TP MAZEMBE YAUSHINDWA MUZIKI WA WAJAPAN,YAPIGWA GOLI ZA KUTOSHA NA KUPOTEZA NAFASI YA KUIVAA RIVER PLATE

Osaka,Japan.

Ndoto za Watanzania kuwaona nyota wao Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wakifika mbali katika michuano ya vilabu bingwa duniani inayoendelea nchini Japan imeyeyeka mchana wa leo baada ya TP Mazembe kukubali kichapo cha magoli 3-0 toka kwa Sanfrecce Hiroshima ya Japan katika mchezo mkali wa robo fainali uliopigwa huko Osaka.

Sanfrecce Hiroshima imejipatia magoli yake dakika ya 44,56 na 78 kupitia kwa Tsukasa Shiotani,Kazuhiko Chiba na Takuma Asano.

Kufuatia ushindi huo Sanfrecce Hiroshima itavaana na River Plate ya Argentina katika mchezo wa nusu fainali huku TP Mazembe siku ya jumanne ikivaana na Club America ya Mexico kusaka nafasi ya tano.

 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: KOMBE LA DUNIA LA VILABU:TP MAZEMBE YAUSHINDWA MUZIKI WA WAJAPAN,YAPIGWA GOLI ZA KUTOSHA NA KUPOTEZA NAFASI YA KUIVAA RIVER PLATE Rating: 5 Reviewed By: Unknown