728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, May 05, 2016

    NG'OLO KANTE KUPEWA JUKWAA UFARANSA

    Boulogne,Ufaransa.

    Klabu ya Boulogne iliyoko ligi daraja la tatu nchini Ufaransa inapanga kulipa jina la N'Golo Kante jukwaa moja la uwanja wake wa nyumbani wa Stade de la Libération kama ishara ya kuenzi mafanikio ya kiungo huyo wa Leicester City ambaye hivi karibuni ametwaa ubingwa wa Ligi Kuu nchini England.(sokaextra.blogspot.com)

    Kante,25 alijiunga na Boulogne akiwa kinda wa miaka 19 na kuichezea kuanzia mwaka 2011 mpaka 2013 kabla ya kujiunga na klabu ya daraja la pili ya Caen wakati huo kwa sasa iko daraja la kwanza maarufu kama [Ligue 1].

    Mkurugenzi mkuu wa Boulogne Nicolas Durand ameliambia gazeti la The Sun "Kante,25 alikuwa na sisi hapa miaka mitatu iliyopita akicheza mbele ya mashabiki 2,000 tu,leo ametwaa ubingwa wa ligi kubwa duniani kwanini tusienzi mafanikio hayo?Alihoji.

    Ni kawaida yetu kuenzi kile kizuri ambacho wachezaji wetu wamefanya wawe hapa hapa ama katika vilabu vingine.

    "Mfano [Franck] Ribery ni shujaa mkubwa Boulogne kwa sababu alizaliwa hapa na akachezea hapa.Ana jukwaa lake hapa,tunataka kufanya hivyo kwa Kante pia kwani amefanya mambo makubwa ndani ya kipindi kifupi."Alimaliza Durand.

    Kante alijiunga na Leicester City Juni 2015 kwa ada ya £8m akitokea klabu ya Caen ambayo nayo ilimsajili kutoka klabu ya Boulogne iliyoko ligi daraja la tatu nchini Ufaransa.

    Nyota wengine maarufu waliowahi kuichezea Boulogne iliyoanzishwa mwaka 1898 ni Lucien Leduc,Daniel Moreira,Yves Triantafyllos,Diafra Sakho,Ovidy Karuru na Frank Ribery.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: NG'OLO KANTE KUPEWA JUKWAA UFARANSA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top