Shinyanga,Tanzania.
Katibu Mkuu wa zamani wa klabu ya Yanga Dkt. Jonas Tiboroha amepata dili jipya kunako klabu ya Stand United ya mkoani Shyinyanga.
Tiboroha anakuwa Mkurugengenzi Mtendaji Mkuu (C.E.O) wa Stand United kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na uongozi wa klabu hiyo iliyoanzishwa mwaka 2012.
Taarifa kutoka ‘Chama la wana’ inasomeka kama ifuatavyo: “Confirmed Tiboroha sasa ni C.E.O wa Stand United, ungana nami kumpongeza na kumtakia kila la kheri katika kazi yake. Tutamtambulisha kwa waandishi
wa habari siku ya Ijumaa kwenye ukumbi wa mikutano wa wadhamini wetu ACACIA”.
Tiboroha alijiuzulu nafasi ya Ukatibu Mkuu katika klabu ya Yanga akitoa sababu ya kuzongwa na majukumu mengi kutoka kwa mwajiri wake ‘mama’ ambaye ni Serikali kupitia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
0 comments:
Post a Comment