728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, May 04, 2016

    SHABIKI AFARIKI BAADA YA KUISHUHUDIA TIMU YAKE IKIPOTEZA MCHEZO

    Accra,Ghana.

    Shabiki mkubwa wa soka nchini Ghana Yahaya “Alhaji Car” amefariki dunia Jana Jumanne baada ya kushindwa kuvumilia uchungu wa kuishuhudia klabu yake kipenzi ya Hearts of Oak ikichapwa bao 1-0 na wapinzani wao wa jadi klabu ya Kumasi Asante Kotoko katika mchezo mkali wa Ligi Kuu ya Ghana uliochezwa Jumatatu jioni huko Accra Sports Stadium .

    Taarifa kutoka nchini Ghana zinasema Yahaya alidondoka na kisha kuzirai kabla ya kuwahishwa hospitalini kwa ajili ya kupatiwa matibabu lakini masaa 24 baadae yaani Jumanne asubuhi alitangazwa kuwa amefariki dunia.

    Kwa mujibu wa mashuhuda wetu inasemeka Yahya alipatwa na shambulio la moyo baada ya mlinda mlango wa Hearts of Oak Soulama Abdoulaye kufanya kosa la kizembe lililoipatia ushindi wa bao hilo moja klabu yake ya zamani ya Kumasi Asante Kotoko.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SHABIKI AFARIKI BAADA YA KUISHUHUDIA TIMU YAKE IKIPOTEZA MCHEZO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top