728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, May 04, 2016

    LICHA YA KUTWAA UBINGWA WACHEZAJI SITA WA LECEISTER CITY KUTOPEWA MEDALI KISA KIKO HAPA

    Leceister,England.

    Wakati Leceister City wakikaribia kukabidhia ubingwa wao wa Ligi Kuu England sokaextra.blogspot.com imegundua kuwa wachezaji sita wa klabu hiyo hawatapewa medali za ubingwa hii ni kutokana na ukweli kwamba wachezaji hao hawajafikia idadi ya michezo inayotakiwa ili waweze kupata haki hiyo.

    Kwa mujibu wa sheria za sasa za FA ni kuwa mchezaji anayepaswa kupewa medali ya ubingwa wa Ligi Kuu ni yule tu aliyecheza kuanzia michezo mitano na kuendelea.

    Hii ina maana kwamba wachezaji walicheza michezo pungufu kuanzia minne na kushuka chini hawatapata medali ya ubingwa.

    Je,Leceister City wanapaswa kufanya nini ili wachezaji wao wote wapate Medali??

    Wanapaswa kuzinunua.Msimu uliopita wakati Chelsea wanakaribia kutawazwa kuwa mabingwa wa Ligi Kuu Kocha Jose Mourinho alilazimika kutoa pesa kwa ajili ya kuwanunulia medali wachezi ambao hawakuwa wamefikisha idadi ya michezo mitano ya Ligi Kuu.

    Hivi ndivyo Leceister City watakapaswa pia kufanya vinginevyo wachezaji wake sita akiwemo mlinda mlango wake mkongwe Mark Schwarzer,43 hawatapata medali za ubingwa.

    WACHEZAJI WATAKAOPATA MEDALI ZA UBINGWA NI:(Kwenye mabano ni idadi ya Mechi walizocheza)

    1.Kasper Schmeichel (36)
    2.Wes Morgan (36)
    3.Marc Albrighton (36)
    4.N'Golo Kante (35)
    5.Riyad Mahrez (35)
    6.Robert Huth (35)
    7.Shinji Okazaki (34)
    8.Danny Drinkwater (34)
    9.Jamie Vardy (34)
    10.Christian Fuchs (30)
    11.Leonardo Ulloa (28)
    12.Danny Simpson (28)
    13.Andy King (23)
    14.Jeff Schlupp (22)
    15.Nathan Dyer (12)
    16.Demarai Gray (10)
    17.Gokhan Inler (5)
    18.Daniel Amartey (5)

    WACHEZAJI WATAKAOKOSA MEDALI ZA UBINGWA NI: (Kwenye mabano ni idadi ya Mechi walizocheza)

    1. Marcin Wasilewski (2)
    2. Mark Schwarzer (0)
    3. Ben Chilwell (0)
    4. Liam Moore (0)
    5. Matty James (0)
    6. Ben Hamer (0)

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: LICHA YA KUTWAA UBINGWA WACHEZAJI SITA WA LECEISTER CITY KUTOPEWA MEDALI KISA KIKO HAPA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top