728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, May 04, 2016

    MBWANA SAMATTA AMTETA NGOMA

    Donald Ngoma

    Genk, Ubelgiji. 

    STRAIKA Mtanzania anayekipiga Klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta,ameshindwa kuficha hisia zake na kummwagia sifa mshambuliaji wa Yanga,Mzimbabwe Donald Ngoma kuwa jamaa anajua.

    Ngoma amesajiliwa na Yanga msimu huu akitokea timu ya FC Platinum ya Zimbabwe na ameonyesha kiwango kizuri kiasi cha kuwakuna mashabiki wengi wa soka nchini.

    Samatta amekuwa akilifuatilia soka la hapa nyumbani kupitia mitandaoni kwa kuangalia mechi zinazochezwa hapa Tanzania katika ligi zote.

    Straika huyo alisema licha ya kuipenda Simba lakini amekuwa akivutiwa zaidi na jinsi ambavyo Ngoma anajituma uwanjani kutafuta ushindi kwa timu yake.

    “Mimi naipenda Simba.Lakini anajua na tena anajituma sana, hivyo yeyote yuleanayejua na kufuatilia soka nina imani ana kila sababu ya kumpongeza,” alisema Samatta ambaye kwa sasa anafanya vizuri katika klabu yake hiyo ya Genk, 



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MBWANA SAMATTA AMTETA NGOMA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top