LONDON,ENGLAND.
MABAO matatu ya Mfaransa Olivier Giroud yameipeleka Arsenal mpaka nafasi ya pili ya msimamo wa Ligi Kuu England baada ya leo jioni kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Arsenal katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Emirates jijini London.
Bao jingine la Arsenal limepatikana baada ya mlinzi wa Aston Villa Mark Bunn kujifunga akiwa katika harakati za kuokoa mkwaju wa nahodha Mikel Arteta.
Kwa ushindi huo Arsenal imepanda mpaka nafasi ya pili baada ya kufikisha pointi 71 na kuishuka Tottenham mpaka nafasi ya pili baada ya kubaki na pointi zake 70 kufuatia kufungwa na Newcastle United.
Newcastle United ikiwa nyumbani St.James Park imeichapa Tottenham kwa mabao 5-1,Watford imetoka sare ya 2-2 na Sunderland.
Huko St.Mary wenyeji Southampton wameichapa Crystal Palace kwa mabao 3-,Liverpool imetoka sare ya 1-1 na West Bromwich Albion.
Everton ikiwa nyumbani Goodson Park imeifunga Norwich City kwa mabao 3-0,huko Brittania Stoke City wameichapa Westham kwa mabao 2-1
Swansea City imetoka sare ya 1-1 na Manchester City.Bao la Swansea City limefungwa na Andre Ayew huku lile la Manchester City likifungwa na Kelechi Iheanacho.
Mabingwa Leceister City wametoka sare ya 1-1 na Chelsea.Wafungaji Cesc Fabregas na Daniel Drinkwater.
0 comments:
Post a Comment