728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, May 15, 2016

    HIZI HAPA HABARI ZA USAJILI NDANI NA NJE YA TANZANIA JUMAPILI YA LEO MEI 15/2016


    Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC Zacharia Hans Poppe amesema klabu hiyo imepanga kukiboresha kikosi chake kwa kusajili nyota wanne wa kigeni katika msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.Pia Hans Poppe amesema kuwa Simba SC itawarudisha kikosini nyota wake wote walioko villabu vingine vya Ligi Kuu kwa mkopo.Baadhi ya nyota hao ni Miraj Athumani na Miraj Adam na Dennis Richard.

    Kavumbagu:Klabu ya Azam imepanga kutema wachezaji 13 wakiwemo wageni na wazawa na kusajili wengine tayari kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.Baadhi ya wachezaji watakaotemwa ni Didier Kavumbagu na Kipre Balous.(Azam.Com)

    Higuain:Mmiliki wa Napoli Aurelio De Laurentiis amesema mshambuliaji wake Muargentina Gonzalo Higuain,28 hawezi kuondoka klabuni hapo kwa dau la chini ya €94m.(Gezzetta dello sport)

    Camacho:Leicester City imeripotiwa kuungana na Liverpool katika mbio za kumuwania kiungo wa Malaga Ignacio
    Camacho mwenye thamani ya £10m.

    Williams:Arsenal imeandaa kitita £20m kwa ajili ya kumsajili mlinzi wa kati wa Swansea City Ashley Williams,31baada mlinzi chaguo la kwanza Mats Hummels kujiunga na Bayern Munich.(Sunday Express)

    Carvajal:Pep Guardiola ameiambia klabu yake mpya ya Manchester City kuhakikisha inamsajili mlinzi wa kulia wa Real Madrid Dani Carvajal.(Sunday People)

    Flamini:Klabu iliyopanda daraja ya Middlesbrough inataka kujiimarisha kwa kumsajili kiungo mkongwe wa Arsenal Mathieu Flamini,33.(Daily Star)

    Borthwick:Mlinzi wa kushoto wa Manchester United Cameron
    Borthwick-Jackson amekubali kuongeza mkataba wa miaka minne wa kuendelea kuitumikia miamba hiyo ya Old Trafford.(Sunday People)

    Mourinho: Everton imejitosa katika mbio za kumuwania kocha Mreno Jose Mourinho baada ya kuripotiwa kuanza nae mazungumzo ya kutaka kumwajiri ili azibe nafasi ya Robert Martinez aliyetimuliwa wiki iliyopita.(The Sunday Times)

    Guardiola:Kocha mpya wa Manchester City Pep Guardiola ameripotiwa kutaka kuvamia katika vilabu vya Arsenal na Tottenham na kuwasajili Jack Wilshere and Alexis Sanchez na mlinzi wa kushoto Danny Rose.(Daily Mirror)

    Murillo:Liverpool imeripotiwa kutaka kuziba pengo la mlinzi wake aliyefungiwa Mamadou Sakho kwa kumsajili mlinzi wa Inter Milan Jason Murillo, 23 anayekadiriwa kuwa na thamani ya £22m.(The People)

    Murillo:Liverpool imeripotiwa kutaka kuziba pengo la mlinzi wake aliyefungiwa Mamadou Sakho kwa kumsajili mlinzi wa Inter Milan Jason Murillo, 23 anayekadiriwa kuwa na thamani ya £22m.(The People)




    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HIZI HAPA HABARI ZA USAJILI NDANI NA NJE YA TANZANIA JUMAPILI YA LEO MEI 15/2016 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top