728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, May 05, 2016

    HABARI NJEMA TANZANIA!!FARID MUSA AFUZU MAJARIBIO HISPANIA

    Tenerife,Hispania.

    WINGA wa kimataifa wa Tanzania,anayekipiga Azam FC Farid Mussa Malik amefuzu majaribio ya kucheza soka la kulipwa katika klabu ya Deportivo Tenerife ya Ligi Daraja la pili nchini Hispania maarufu kama Segunda B.

    Habari hiyo njema kwa soka la Tanzania imeripotiwa na Mkurugenzi wa Azam FC, Yussuf Bakhresa anayefuatilia majaribio ya mchezaji huyo huko Hispania,.

    Kilichobaki sasa ni vilabu vya CD Tenerife na Azam FC kukaa mezani na kufanya mazungumzo juu ya kuuziana mchezaji huyo anayekipiga pia Taifa Stars.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HABARI NJEMA TANZANIA!!FARID MUSA AFUZU MAJARIBIO HISPANIA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top