RIJEKA, Croatia.
CROATIA imepata ushindi wake mkubwa wa kwanza baada ya Jumamosi usiku kuichapa San Marino mabao 10-0 katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki wa kujiandaa na Euro uliochezwa huko Rijeka,Croatia.
Mpaka mapumziko Croatia ilikuwa inaongoza kwa mabao 6-0 kupitia kwa Mario Mandzukic aliyekuwa amefunga mabao matatu ndani ya dakika 14 (24,36 na 38) mengine yakifungwa na Marko Pjaca, Darijo Srna na Ivan Perisic.
Kipindi cha pili Croatia iliongeza mabao mengine manne kupitia kwa Nikola Kalinic aliyefunga mara tatu na Ivan Rakitic aliyefunga mara moja.
Katika mchezo huo Croatia ilipiga mashuti 27 langoni huku wapinzani wao San Marino wakishindwa kupiga hata shuti moja.
Croatia itaanza kidumbwendumbwe kwa Euro kwa kucheza na Uturuki June 12 huko Paris.
0 comments:
Post a Comment