Shirikisho la soka barani Africa Caf Leo mchana limepiga kura ya kuipitisha uanachama wa Caf Zanzibar na kupita bila kipingamizi chochote kwa kupata kura zote za wajumbe wa mkutano mkuu.
Rais wa Chama cha soka Tanzania Jamal Malinzi aliahidi kuifikisha Zanzibar kwenda kutambulika na Car na amefanikiwa kwa hilo
Kwa sasa rasmi kabisa Zanzibar ni mwanachama halali wa Caf na amepewa namba 55 ya uanachama wa Caf
Sasa Zanzibar itafaidika na fedha za maendeleo mbali mbali ya kimichezo kutoka Caf moja kwa sio kama zamani isubilie mgao toka TFF .Mgao huo ni kama maendeleo ya soka la vijana , wakinamama , msaada wa ujenzi wa viwanja mbali mbali na pia Zanzibar wanasubili kupitishwa pia kama mwanachama halali wa Fifa punde 2 watapopeleka maombi yap.
Soka extra blog inaitakia kila la kheri Zanzibar .
0 comments:
Post a Comment