728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, March 16, 2017

    Hatimaye , Hans Van der Pluijm kutimukia Singida United


    Aliyewahi kuwa Kocha wa Dar es salaam Young African ( Yanga ) kwa vipindi viwili tofauti na pia ndio aliyekuwa mkurugenzi wa ufundi wa Yanga Hans van der Pluijm.

    Ameoneka akishiliki kwenye usajili wa mchezaji mpya wa timu ya Singida United  kumsajili kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Zimbabwe,Tafadzwa Raphael Kutinyu.

    Taarifa zilizotufikia Soka Extra blog ni kuwa klabu hiyo iko mbioni kukamilisha usajili wa Kocha huyo wa zamani wa yanga Hans Pluijm na punde baada ya kukamilika kwa usajili huo utawekwa wazi .

    Nukuu " tumefanya mazungumzo na Kocha Hans na yuko Tayali kubaki Tanzania ila kuna mambo kidogo ya kiutawala hatujayaweka sawa ndo maana tunasita kutangaza kuwa tumsajili Kocha Hans " Soka extra ilipozungumza na mmoja wa kiongozi wa Singida United hakutaka kutajwa jina

    Na alipoulizwa kuhusu kuendelea na usajili alisema bado wapo mbioni kudaka saini za nyota wengine wa kimataifa haswa kutoka Zambia na Wengine wa hapa hapa nchini ili kuimalisha timu yao ya Singida united.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Hatimaye , Hans Van der Pluijm kutimukia Singida United Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top