728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, March 16, 2017

    Nyota wa AFCON atua Singida United

    Singida,Tanzania.

    TIMU ya soka ya Singida United ambayo hivi karibuni imerejea ligi kuu Tanzania bara baada ya kupoteza kwa miaka mingi imeanza kukiimarisha kikosi chake tayari kwa msimu ujao hii ni baada ya jana Jumatano kumsajili kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Zimbabwe,Tafadzwa Raphael Kutinyu.

    Kutinyu mwenye umri wa miaka 22 amejiunga na Singida United kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Chicken Inn ya nyumbani kwao Zimbabwe kwa ada ambayo haijawekwa wazi.



    Akiwa na Chicken Inn, mwaka 2016 Kutinyu aliiwezesha timu hiyo kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Zimbabwe.Kutinyu pia amekuwa mhimili mkubwa kwenye timu ya taifa ya Zimbabwe tangu alipoitwa kwa mara ya kwanza mwaka 2015.Alikuwemo pia kwenye kikosi kilichokwenda nchini Gabon kushiriki michuano ya AFCON 2017.

    Kutinyu alizaliwa Disemba 22,1994 na ni mume wa mrembo Portia Tsitsidzashe waliyefunga ndoa Agosti 2016.Mwaka 2014 akiwa na Bantu Rovers,Kutinyu alipata nafasi ya kwenda nchini Ubelgiji kufanya majaribio Club Brugge lakini kwa bahati mbaya hakufanikiwa.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Nyota wa AFCON atua Singida United Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top