728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, March 30, 2017

    Marefa wa Rwanda, Guinea kuchezesha Yanga na MC Alger

    Faridi Miraji , Dar es salaam.                         


    SHIRIKISHO ya Soka Afrika (CAF), limewateua marefa wa Rwanda na Guinea kuchezesha mechi mbili za mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Yanga SC na MC Alger ya Algeria.

    Mchezo wa kwanza Aprili 8, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam utachezeshwa na Louis Hakizimana Atakayepuliza Filimbi Akisaidiwa Na Theogene Ndagijimana na Jean Bosco Niyitegeka wote kutoka Rwanda.

    Mchezo wa marudiano Aprili 14 nchini Algeria utachezeshwa na marefa wa Guinea, ambao ni Yakhouba Keita, Aboubacar Doumbouya na Mamady Tere na mshindi wa jumla atafuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika mwaka huu.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Marefa wa Rwanda, Guinea kuchezesha Yanga na MC Alger Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top