728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, March 26, 2017

    Singida United yaongeza wakali wawili kutoka Zimbabwe


    Paul Manjale.

    WAGENI kwenye ligi kuu ya Tanzania,Singida United wameendelea na mikakati ya kukiimarisha kikosi chao tayari kwa msimu ujao wa ligi hiyo baada ya jioni ya leo kukamilisha usajili wa wachezaji wawili wa kimataifa kutoka nchini Zimbabwe,Elisha Muroiwa,27 na Wisdom Mtasa,22.

    Wachezaji hao wanaotokea Power Dynamos wamesaini mkataba wa miaka miwili miwili wa kuitumikia Singida United ilipanda ligi kuu msimu huu baada ya kushuka takribani miaka 12 iliyopita.

    Kabla ya kuwanasa wachezaji hao wawili wanaoichezea pia timu ya taifa ya Zimbabwe tayari Singida United ilikuwa imeshamsajili kiungo mshambuliaji wa CAPS United ya Zimbabwe,Tafadwaza Kutinyu.




    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Singida United yaongeza wakali wawili kutoka Zimbabwe Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top