James Eduma,Iringa
Mkuu wa idara ya habari na mawasilino wa klabu ya Simba Haji
Manara, kwa mara ya kwanza amefichua siri ya kilichosababisha kufungiwa kwa
aliyekua msemaji wa klabu ya Young Africans Jerry Muro.
Manara amesema alichangia kufungiwa kwa Jerry Muro kwa kutumia
udhaifu wa shirikisho la soka nchini TFF, ambalo kwa asilimia kubwa lilionekana
kumfumbia macho Jerry Muro pale alipoonyesha kukosea kwa kutoa lugha ambazo
hazikua za kiungwana katika michezo.
Manara amesema alifanya mchezo huo kwa kutumia elimu aliyowahi
kuipata nchini China.
Hata hivyo Haji Manara amekiri kumiss Jerry Muro katika shughuli
za usemaji wa klabu za Simba na Young Africans japo akaendelea kusisitiza rafiki
yake alikosea kusimamia misingi ya mchezo wa soka ambayo inakataza maneno ya
kashfa na kejeli.
0 comments:
Post a Comment