Dar Es Salaam,Tanzania.
Beki kisiki wa Simba Method Mwajale jumamosi hii anatarajiwa kuanza mazoezi na wenzake kujiandaa na mechi za ligi kuu zinazofuata.
Mwajale alikuwa nje ya uwanja kutokana na majeruhi ya goti aliyoyapata Februari 11 kwenye mechi ya ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons iliyochezwa Dar Es Salaam na Simba kuibuka na Ushindi wa magoli 3-0. Mwajale Amekosa Michezo saba mpaka sasa ikiwa miwili ya ligi kuu, michezo miwili ya kombe la Azam Sports Federation Cup na michezo mitatu ya kirafiki.
Dktari wa Simba, Yassin Gembe amedhibitisha kuwa Mwajale kwa sasa yuko fiti kuanza mazoezi na wenzake. Tuliamua kumpumzisha Kwa muda mrefu ili awe fiti kabisa na sasa Jumamosi Hii ataungana na timu kwenye mazoezi ya kujiandaa na mechi za Kanda ya ziwa.
Kocha Msaidizi wa Simba Jackson Mayanja amesema ni furaha sana kurejea Kwa Method atatusaidia sana kwenye kuwania ubingwa wa ligi kuu tumebakiza mechi chache inatakiwa wachezaji kuwa fiti ili kupambana Kwa asilimia zote.
0 comments:
Post a Comment