Carvalho:Real Madrid inaandaa kitita cha €45m ili kumsajili kiungo mahiri wa Sporting ya Ureno William Carvalho,21.Real Madrid imezidisha kasi baada ya Sporting Lisbon kumsajili Muitaliano Alberto Aquilani.
Otamendi:Manchester City iko tayari kutoa kitita cha pesa pamoja na mlinzi wake Eliaquim Mangala ili kumsajili mlinzi wa Valencia Nicolas Otamendi. (Daily Mirror)
Berahino:Baada ya kumuuza mshambuliaji wake Roberto Soldado kwenda Villarreal Tottenham inaandaa kitita cha £15m kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa West Brom Saido Berahino,21.Hata hivyo mpango huo huenda ukakwama kwani West Brom imeendelea kusisitiza haitamwachia nyota huyo kwa dau la chini ya £25m.(Daily Telegraph)
Burak:West Ham imeendelea kusaka mshambuliaji mpya na safari hii jicho lake limetua kwa mshambuliaji wa Galatasaray Burak Yilmaz,30.West Ham imeandaa kitita cha €10 ili kumnasa mkali huyo wa mabao tuko Uturuki.(Metro)
Destro:Norwich City ina matumaini makubwa ya kuipiku Bologna katika mbio za kuinasa saini ya mshambuliaji wa AS Roma Mattia Destro,24. (Norwich Evening News)
Illarramendi:Liverpool iko katika nafasi nzuri ya kumsajili kiungo Asier Illarramendi,25 baada ya Real Madrid kuwa tayari kumuuza nyota huyo wa zamani wa Real Sociedad.(Metro)
0 comments:
Post a Comment