728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, August 15, 2015

    ASHLEY COLE ATUPIWA VIRAGO AS ROMA,MSHAHARA MKUBWA WAMPONZA

    Roma,Italia.

    Maisha ya mlinzi mkongwe Ashley Cole ndani ya klabu ya AS Roma yamekuwa mafupi kuliko ilivyotarajiwa baada ya nyota huyo wa zamani wa vilabu vya Arsenal na Chelsea kutupiwa virago na miamba hiyo ya Italia.

    Cole,34 ambaye alijiunga na AS Roma msimu uliopita kwa mkataba wa miaka miwili kama mchezaji huru akitokea Chelsea ametupiwa virago baada ya kufikia makubaliano ya kufanya hivyo.

    Roma imefikia hatua hiyo baada ya kuona inapata hasara kwa kumlipa Cole mshahara mkubwa wakati hana msaada katika timu.Msimu uliopita Cole alifanikiwa kucheza jumla ya michezo 11 pekee huku kila wiki akiweka kibindoni kitita cha £35,000 ambacho kwa ligi ya Seria A ni kikubwa.

    Cole hakutajwa katika kikosi cha wachezaji 26 wa As Roma waliokuwa wakitambulishwa jana ijumaa katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Sevilla.Kati ya majina mapya katika utambulisho huo uliofanyika Stadio Olympico ni Wojciech Szczesny, Mohamed Salah na Edin Dzeko

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: ASHLEY COLE ATUPIWA VIRAGO AS ROMA,MSHAHARA MKUBWA WAMPONZA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top