Zagreb,Croatia.
WACHEZAJI wa timu ya taifa ya vijana ya England ya chini ya umri wa miaka 17 wakipongezana baada ya Jumanne usiku kuwafunga vijana wenzao wa Uturuki mabao 2-1 katika mchezo wa nusu fainali ya michuano ya Ulaya huko NK Varaždi,Croatia.
Mabao yaliyoipeleka England fainali yamefungwa na Callum Hudson-Odoi anayechezea kikosi cha vijana cha Chelsea pamoja na Jadon Sancho wa kikosi cha vijana cha Manchester City.
Aidha mchezo huo ulilazimika kusimama kwa dakika 15 kupisha madaktari kumpatia matibabu ya dharura Tashan Oakley-Boothe wa England aliyekuwa amepoteza fahamu baada ya kugongana na Hasan Adiguzel wa Uturuki.
Katika mchezo wa nusu fainali ya pili imeshuhudiwa Hispania ikiiondosha mashindanoni Ujerumani kwa penati 4-2 baada ya sare ya 0-0.Fainali itachezwa Ijumaa kwenye uwanja wa NK Varaždi.
Ikiwa England itashinda ubingwa Ijumaa itakuwa ni timu ya kwanza kushinda ubingwa huo mara ya tatu baada ya mwaka 2010 na 2014.
0 comments:
Post a Comment