Leceister, England.
Leicester City imeendelea kuukaribia ubingwa wa kwanza wa ligi kuu England baada ya leo mchana kuifunga Southampton kwa bao 1-0 huko King Power.
Bao pekee la mchezo huo limefungwa kwa kichwa dakika ya 38 na nahodha Wes Morgan akiunganisha krosi ya mlinzi Chriatian Fuchs toka wingi ya kushoto.
Kufuatia ushindi huo Leceister City imeendelea kung'ang'ania kileleni baada ya kufikisha pointi 69 baada ya kushuka dimbani mara 32.
0 comments:
Post a Comment