Dar es salaam,Tanzania.
Yanga imeendelea kuipumuFCC 0-0a Simba kileleni mwa msimamo wa ligi kuu Tanzania bara baada ya jioni ya leo kuifunga Kagera Sugar kwa mabao 3-1 katika mchezo mkali uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es salaam.
Mabao yaliyoipa ushindi Yanga leo hii yameifungwa na Donald Ndombo Ngoma (29),Amissi Tambwe (62) na Mwinyi Hajji Mgwali kwa kichwa dakika ya 89 akiunganisha krosi safi ya Simon Msuva.
Bao la Kagera Sugar limefungwa na Mbaraka Yussuph dakika ya 9 ya kipindi cha kwanza akimalizia krosi safi ya mlinzi Salum Kanoni aliyepata kusaidia mashambulizi.
Huko CCM Kirumba Mwanza Azam FC imelazimishwa sare ya 1-1 na Toto Africans.
Matokeo mengine
Stand United 2-0 Jkt Mgambo
Ndanda FC 0-0 Prisons
Jkt Ruvu 1-0 African Sports
0 comments:
Post a Comment