Manchester, England.
Ikiwa nyumbani Old Trafford Manchester United imefufua matumaini ya kucheza ligi ya mabingwa msimu ujao baada ya jioni ya leo kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wageni Everton.
Bao pekee la mchezo huo limetiwa kimiani Kipindi cha pili na mshambuliaji Mfaransa Antony Martial.
Martial amefunga bao hilo dakika ya 56 akiunganisha krosi safi ya kinda Timothy
Fosu-Mensah na kuipeleka Manchester United mpaka nafasi ya tano ya msimamo wa ligi kuu England ikiwa na pointi zake 53 baada ya kushuka dimbani mara 31.
Bao hilo la Martial limekuwa ni bao la 1,000 kufungwa na mchezaji wa Manchester United katika dimba la Old Trafford tangu kuanza Kwa ligi kuu mwaka 1992.
0 comments:
Post a Comment