728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, April 04, 2017

    Ligi kuu Indonesia yazidi kuvutia mastaa,baada ya Michael Essien sasa ni zamu ya Peter Odemwingie


    Jakarta,Indonesia.

    WINGA wa zamani wa Nigeria,Peter Osaze Odemwingie amejiunga na klabu ya Madura United inayoshiriki ligi kuu nchini Indonesia kwa mkataba ambao haujawekwa wazi.

    Odemwingie,35,aliyewahi kutamba na vilabu vya La Louvière, Lille, Lokomotiv Moscow,West Bromwich Albion, Cardiff City, Stoke City na Bristol City amejiunga na Madura United akiwa mchezaji huru baada ya mwezi Januari kuachana na Rotherham United ya nchini England.


    Odewingie atakuwa akivalia jezi namba 24 katika kipindi chote atakachokuwa akiitumikia miamba hiyo ya Gelora Ratu Pamelingan.

    Odewingie anakuwa mchezaji wa tatu mwenye jina kubwa kutua ligi kuu nchini Indonesia baada ya Micheal Essien na Carlton Cole ambao kwa nyakati tofauti walitamba ligi kuu England.

    Ligi kuu nchini Indonesia inatarajiwa kuanza kutimua vumbi lake Aprili 15 mwaka huu na itakuwa ikishirikisha vilabu 16 wakiwemo mabingwa wa msimu uliopita Persipura.




    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Ligi kuu Indonesia yazidi kuvutia mastaa,baada ya Michael Essien sasa ni zamu ya Peter Odemwingie Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top