Paul Manjale,Dar Es Salaam
KLABU ya Mbeya City inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Tanzania maarufu kama Ligi Kuu Bara imeingia kandarasi ya miaka miwili ya udhamini na kampuni ya kutengeneza vifaa vya michezo ya Sports Masters ya jijini Dar Es Salaam.
Utiaji saini wa kandarasi hiyo mbayo haijawekwa wazi ni ya kiasi gani ulifanyika jana Jumamosi kwenye ukumbi wa hoteli ya Hill View iliyopo jijini Dar Es Salaam.
Kandarasi hiyo imeipa Sports Masters haki ya kuwa Mtengenezaji na Msambazaji mkuu wa vifaa vyote vya michezo vitakavyokuwa na nembo ya klabu hiyo iliyoanzishwa mwaka 2009 huko jijini Mbeya.
0 comments:
Post a Comment