Paris,Ufaransa.
EDINSON Cavani amefunga bao lake la 44 la msimu baada ya Jumamosi usiku kuingoza Paris Saint-Germain kuichapa Montpellier mabao 2-0 katika mchezo mkali wa ligi daraja la kwanza Ufaransa (Ligue 1) uliochezwa huko Parc des Princes,Paris.
Cavani aliifungia Paris Saint-Germain bao la kuongoza katika dakika ya 29 ya kipindi cha kwanza baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa kiungo wa kimataifa wa Ufaransa,Blaise Matuidi na kufikisha mabao 31 Ligue 1.
Cavani aliiendelea kuonyesha soka safi baada ya Pasi yake ya kisigino kumkuta Angel Di Maria aliyeifungia Paris Saint-Germain bao la pili katika dakika ya 48 ya kipindi cha pili.Bao hilo limemfanya Di Maria afikishe mabao matano katika michezo mitano iliyopita.
Ushindi huo umeifanya Paris Saint-Germain ikwee kileleni mwa msimamo wa Ligue 1 na kuwashusha waliokuwa vinara wa muda mrefu,AS Monaco ambao wana michezo miwili pungufu na leo jioni watakuwa ugenini kucheza na Lyon.
0 comments:
Post a Comment