728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, April 15, 2017

    UZUSHI:Cristiano Ronaldo na kashfa ya ubakaji


    Madrid,Hispania.

    STAA wa Real Madrid Mreno,Cristiano Ronaldo ameibuka na kupinga kwa nguvu zote taarifa zinazodai kuwa Julai 13,2009 alimbaka mwanamke mmoja wa kizungu huko jijini Las Vegas nchini Marekani.

    Jana Ijumaa jarida la Ujerumani la Der Spiegel lilichapisha habari kuwa Ronaldo,32,alifanya shambulizi la kingono dhidi ya mwanamke mmoja kwenye chumba cha hoteli yake ya Sin City iliyoko jijini Las Vegas.

    Der Spiegel limeongeza kuwa Ronaldo alimpa mwanamke huyo Dola 375,000 ili kumziba mdomo katika makubaliano yaliyofikiwa Januari 12,2010 na kuhifadhiwa kimaandishi katika waraka wa kurasa tatu.Waraka huo umedaiwa kuwa ulimtaka mwanamke huyo kutoliongelea jambo hilo hadharani.

    Ronaldo kupitia kwa mwanasheria wake,Carlos Osorio de Castro amedai kuwa taarifa hizo ni za uzushi na zinalenga kumchafulia jina na kuongeza kuwa atapamba kadri ya uwezo wake kuhakikisha jambo hilo linakwisha salama.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: UZUSHI:Cristiano Ronaldo na kashfa ya ubakaji Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top