Leceister,England.
LIGI ya mabingwa Ulaya inatarajiwa kuendelea tena leo kwa michezo miwili ya marudiano ya hatua ya robo fainali kuchezwa katika miji ya Leceister (England) na Madrid (Hispania).
Katika mchezo wa kwanza mabingwa watetezi wa ligi kuu nchini England, Leceister City watakuwa nyumbani King Power wakipambana kuweka rekodi ya kufuzu nusu fainali ya michuano hiyo kwa mara ya kwanza pale watakapowakaribisha Atletico Madrid.
Ikumbukwe katika mchezo wa awali uliochezwa Jumatano iliyopita huko Vincente Cardelon,Leceister City walikubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Atletico Madrid.Ili waweze kufuzu nusu fainali Leceister City inahitaji kupata ushindi wa mabao 2-0 na kuendelea huku wapinzani wao Atletico Madrid wakihitaji kupata sare ya aina yoyote ile.
Katika mchezo wa pili Real Madrid wakiwa bila ya staa wao,Gareth Bale anayesumbuliwa na majeruhi ya mguu watakuwa nyumbani Santiago Bernabeu kuwaalika mabingwa wa Ujerumani,Bayern Munich ambao wametiwa chachu kwa urejeo wa mshambuliaji wao mahiri Robert Lewandowski aliyeukosa mchezo wa kwanza kutokana na kuwa majeruhi.
Real Madrid wanaingia katika mchezo wa leo wakihitaji sare ama ushindi wowote ule ili waweze kufuzu nusu fainali kwa msimu wa saba mfululizo.Bayern Munich wao wanaingia katika mchezo wa leo wakihitaji ushindi wa kuanzia mabao 2-0 na kuendelea.Mara ya mwisho Bayern Munich kuifunga Real Madrid ilikuwa ni mwaka 2001pale ilipoichapa kwa bao 1-0 lililofungwa na Mbrazil,Giovane Elber.
Ratiba Kamili
Leceister City v Atletico Madrid
Real Madrid v Bayern Munich
Michezo yote itaanza saa 9:45 usiku.
0 comments:
Post a Comment