728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, April 17, 2017

    TP Mazembe,wababe wa Azam FC watinga makundi kombe la shirikisho Afrika


    Algiers,Algeria.

    MABINGWA wa msimu uliopita wa kombe la shirikisho barani Afrika,TP Mazembe ya DR Congo, wamefanikiwa kutinga hatua ya makundi ya michuano hiyo kwa mara ya pili mfululizo baada ya jana Jumapili usiku kutoka sare ya bila kufungana na JS Kabylie ya Algeria katika mchezo wa marudiano uliochezwa huko jijini Algiers,Algeria.

    Ikumbukwe katika mchezo wa awali uliochezwa Jumapili iliyopita huko Lubumbashi ,TP Mazembe waliifunga JS Kabylie kwa jumla ya mabao 2-0.Hivyo wamefuzu makundi kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-0.

    Wakati huohuo Mbabane Swallows imeweka historia ya kuwa timu ya kwanza kutoka Swaziland kutinga hatua ya makundi ya kombe la shirikisho Afrika baada ya kuibanjua AC Leopards ya DR Congo mabao 4-2.Katika mchezo wa awali AC Leopards ilishinda kwa bao 1-0.

    Ikumbukwe Mbabane Swallows ilitinga hatua ya pili ya kombe la shirikisho Afrika baada ya kuing'oa Azam FC ya Tanzania kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-1.Katika mchezo wa awali uliochezwa Chamazi, Mbabane Swallows ililala kwa bao 1-0 la Ramadhani Singano 'Messi'.

    Katika mchezo mwingine ASEC Mimosas ya Ivory Coast imetupwa nje ya michuano hiyo na CF Mounana ya Gabon baada ya kulazimishwa sare ya 0-0.Katika mchezo wa awali ASEC Mimosas ililala kwa mabao 2-1.

    Al Hilal Obeid ya Sudan imeifunga Ports Authority ya Gambia mabao 3-0 na kufuzu kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-1 baada ya kutoka sare ya bao 1-1 katika mchezo wa awali.

    Platinum Stars ya Afrika Kusini imeing'oa michuanoni AS
    Tanda ya Ivory Coast kwa penati 5-4 baada ya sare ya mabao 2-2.

    Baadhi ya timu ambazo zimefanikiwa kufuzu makundi ni pamoja na Rivers Utd (Nigeria),CS Sfaxien (Tunisia),Mbabane Swallows (Swaziland),Zesco Utd (Zambia),Recreativo Libolo (Angola),Club Africain (Tunisia),FUS Rabat (Morocco),Smouha (Egypt),Mouloudia Alger (Algeria),KCCA (Uganda)
    Horoya (Guniea),Platinum Stars (South Africa),CF Mounana (Gabon),SuperSport Utd (South Africa),Al Hilal Obeid (Sudan),TP Mazembe (Congo)

    Droo ya upangaji wa makundi itafanyika Aprili 26 huko Cairo,Misri.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: TP Mazembe,wababe wa Azam FC watinga makundi kombe la shirikisho Afrika Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top