728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, April 29, 2017

    EPL:Arsenal,Man United,Chelsea,Southampton dimbani wikendi hii,ratiba kamili iko hapa


    London,England.

    LIGI KUU ya soka nchini England maarufu kama Premier League inatarajiwa kuendelea tena leo Jumamosi Aprili 29 kwa michezo mitano kuchezwa katika viwanja vitano vya miji mbalimbali.

    Baadhi ya michezo ya leo: Southampton itakuwa nyumbani St.Mary's kupepetana na Hull City. Sunderland ambapo kuna kila dalili kuwa msimu huu watashuka daraja,leo watakuwa wenyeji wa AFC Bournemouth.

    Ligi hiyo itaendelea tena kesho Jumapili Aprili 30 kwa michezo minne kuchezwa ambapo Arsenal itasafiri mpaka White Hart Lane kwenda kuvaana na Tottenham Hotspurs.Vinara wa ligi hiyo Chelsea watakuwa wageni wa Everton huko Goodson Park.

    Kesho kutwa Jumatani Mei 1,2017 Majogoo wa Jiji,Liverpool watakuwa wageni wa Watford huko Vicarage Road.

    Ratika Kamili

    Jumamosi Aprili 29,2017
    Southampton vs. Hull City (17:00)
    Sunderland vs. Bournemouth (17:00)
    Stoke City vs. West Ham (17:00)
    West Brom vs. Leicester City (17:00)
    Crystal Palace vs. Burnley (19:30)

    Jumapili Aprili 30,2017
    Manchester United vs Swansea
    Everton vs Chelsea 
    Middlesbrough vs Manchester City 
    Tottenham vs Arsenal 

    Jumatatu Mei 1,2017
    Watford vs. Liverpool (22:00)


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: EPL:Arsenal,Man United,Chelsea,Southampton dimbani wikendi hii,ratiba kamili iko hapa Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top