London,England.
BAADA ya Juzi Jumapili nahodha wa Real Madrid, Sergio Ramos kulimwa kadi nyekundu ya 22 katika maisha yake ya soka na kuiacha Barcelona ikichomoza na ushindi jadidi wa mabao 3-2 dimbani Santiago Bernabeu kwenye mchezo wa La Liga,mashabiki wa ligi kuu England wametaka kujua ni mchezaji yupi aliyelimwa kadi nyekundu nyingi msimu huu.
Soka Extra kwa msaada ya vyanzo mbalimbali vya habari vya kimataifa tumebaini kwamba Wachezaji Miguel Britos wa Watford,Fernandinho Man City na Granit Xhaka wa Arsenal ndiyo wanaoongoza kwa kulimwa kadi nyingi nyekundu kwa msimu huu ligi kuu England.Wamelimwa kadi mbili mbili kila mmoja.
Wakati huohuo taarifa zinaonyesha kuwa vilabu Everton na Arsenal havijambo kwenye kujikusanyia kadi nyingi nyekundu kwani tangu mwaka 1992 zimekikusanyia kadi nyekundu 169.Everton imejikusanyia kadi nyekundu 86 huku Arsenal ikijikusanyia kadi nyekundu 83.
0 comments:
Post a Comment