London, England.
BAADA ya jana Jumanne usiku kuishuhudia Chelsea ikiifumua Southampton mabao 4-2 nyumbani Stamford Bligde ligi kuu ya soka nchini England (Premier League) inatarajiwa kuendelea tena leo Jumatano kwa michezo mitatu kuchezwa katika viwanja vitatu tofauti huku timu sita zikitoleana makucha kuhakikisha zinajipatia alama tatu muhimu.
Arsenal ambao wako kwenye hatari kubwa ya kushindwa kutinga nne bora msimu huu watakuwa nyumbani Emirates kuwaalika mabingwa watetezi wa ligi hiyo,Leceister City.
Middlesbrough watakuwa nyumbani kwao Riverside kucheza na Sunderland na mchezo wa mwisho leo hii utakuwa kati ya Crystal Palace watakaokuwa nyumbani kwao Selhurts kuwaalika Tottenham.
Ligi hiyo itaendelea tena kesho Alhamis kwa mchezo mmoja kuchezwa ambapo mahasimu wa jiji la Manchester,Manchester City watakuwa uwanjani kwao kupepetana na Manchester United.
Ratika Kamili
Jumatano Aprili 26,2017
Arsenal v Leicester City (9:45 Usiku)
Middlesbrough v Sunderland (9:45 Usiku)
Crystal Palace v Tottenham (10:00 Usiku)
Alhamis Aprili 27,2017
Man City v Man Utd (10:00 Usiku)
Jumamosi Aprili 29,2017
Southampton v Hull City (11:00 Jioni)
Stoke City v West Ham (11:00 Jioni)
Sunderland v Bournemouth (11:00 Jioni)
West Brom v Leicester City (11:00 Jioni)
Crystal Palace v Burnley (1:30 Usiku)
Jumapili Aprili 30,2017
Man Utd v Swansea (8:00 Mchana)
Everton v Chelsea (10:05 Jioni)
Middlesbrough v Man City (10:05 Jioni)
Tottenham v Arsenal (12:30 Jioni)
0 comments:
Post a Comment