Brighton,England
PICHANI ni mashabiki pamoja na wachezaji wa Brighton and Hove Albion wakisherekea kwa furaha baada ya timu hiyo kufanikiwa kurejea ligi kuu England baada ya kujaribu bila mafanikio kwa kipindi cha miaka 34.
Brighton and Hove Albion imerejea ligi kuu England baada ya Jumatatu jioni kuifunga Wigan Athletic kwa mabao 2-1 huko Amex Stadium.Shukrani kwa mabao ya Glenn Murray na Solly March.
Ushindi huo umeifanya Brighton and Hove Albion ifikishe alama 92.Alama saba mbele ya Newcastle United inayoshika nafasi ya pili na alama 13 mbele ya Reading inayoshika nafasi ya tatu.Timu zote zimebakiza michezo minne minne.
Brighton and Hove Albion ambayo mara yake ya mwisho kuonja radha ya daraja la ligi kuu ilikuwa ni msimu wa 1982-83 asa inahitaji kushinda mchezo wake wa Ijumaa ijayo dhidi ya Norwich City ili iweze kutawazwa bingwa wapya wa ligi daraja la kwanza nchini England.
0 comments:
Post a Comment