London,England.
KIUNGO wa Arsenal anayecheza kwa mkopo Bournemouth,Jack Wilshere ameripotiwa kuwa atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi chote kilichobaki cha msimu huu wa ligi kuu nchini England ikibidi na mwanzoni mwa msimu ujao hii ni baada ya kuvunjika mfupa wa fibula kwenye mguu wake wa kushoto.
Wilshere,25,alilazimika kutolewa uwanjani kipindi cha pili kwenye mchezo dhidi ya Tottenham Jumamosi iliyopita baada ya kugongana Harry Kane na kupata jeraha ambalo lilionekana kuwa ni la kawaida.
Lakini baada ya kufanyiwa vipimo vya CT Scan jana Jumanne jioni imebainika kuwa Wilshere amevunjika mfupa wa fibula na hivyo atalazimika kuwa nje ya uwanja kwa kipindi kirefu zaidi.Jeraha hilo linafanana na lile lililomweka nje ya uwanja kwa kipindi kirefu katika msimu wa 2015-16.
Kuumia huko kumekuja kama pigo kwa Wilshere ambaye aliamua kujiunga na Bournemouth mwezi Agosti mwaka jana baada ya kuchoka kusugua benchi Arsenal.
Akiwa na Bournemouth, Wilshere alifanikiwa kucheza michezo 27 idadi ambayo ni kubwa zaidi kwake tangu msimu wa 2013-14.
0 comments:
Post a Comment