728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, April 27, 2017

    Ligi kuu England:Arsenal yahamia mtaa wa sita,yaiachia Everton mtaa wa saba,Spurs inashinda tu


    London, England.

    ARSENAL imeondoka katika nafasi ya saba ya msimamo wa ligi kuu ya soka nchini England na kuweka makazi katika nafasi ya sita baada ya usiku wa leo kuifunga Leceister City kwa bao 1-0 dimbani Emirates.

    Bao pekee lililoamua matokeo ya mchezo huo limebatikana katika dakika ya 86 ya mchezo baada ya mlinzi wa Leceister City,Robert Huth kujifunga akiwa katika harakati za kuokoa shuti la mlinzi wa kushoto wa Arsenal,Nacho Monreal.

    Ushindi huo umeifanya Arsenal ifikishe pointi 60 baada ya kucheza michezo 32.Pointi mbili mbele ya Everton iliyoshuka mpaka nafasi ya saba.Everton imecheza michezo 33.

    Katika mchezo mwingine Tottenham imeibuka na ushindi wa bao 1-0 ugenini kwa kuwafunga wenyeji wao Crystal Palace.Shukrani kwa bao la kiungo Christian Erikssen.

    Middlesbrough wakiwa nyumbani Riverside wameifunga Sunderland kwa bao 1-0 la dakika ya 8 la Roon.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Ligi kuu England:Arsenal yahamia mtaa wa sita,yaiachia Everton mtaa wa saba,Spurs inashinda tu Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top