Madrid,Hispania.
JANA Jumapili usiku Lionel Messi alifunga mabao mawili matata na kuiwezesha Barcelona kuifunga Real Madrid mabao 3-2 katika mchezo safi wa ligi ya La Liga uliochezwa huko Santiago Bernabeu.
Mabao hayo mawili licha ya kuipa Barcelona pointi tatu muhimu bali pia yamemfanya Messi,29,aweke rekodi mbili kubwa.
Kwanza yamemfanya Messi akifishe mabao 16 na kuwa mfungaji bora wa muda wote wa mchezo wa El Classico akimpiku nyota wa zamani wa Real Madrid marehemu, Alfredo Di Stefano mwenye mabao 15.
Pili yamemfanya Messi afikishe mabao 500 akiwa na jezi ya Barcelona aliyoanza kuivaa mwaka 2004 akiwa na umri wa miaka 17.
Mchanganuo wa mabao hayo 500 uko kama ifuatavyo
La Liga: 343
Champions League: 94
Copa Del Rey: 43
Supercopa: 12
Club World Cup: 5
Supercup: 3
JUMLA mabao 500
0 comments:
Post a Comment