728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, April 19, 2017

    Michael Essien anusurika kwenda jela miaka mitano Indonesia.



    Jacarta, Indonesia.

    KIUNGO wa zamani wa Chelsea Mghana,Michael Essien pamoja na mshambuliaji wa zamani wa Westham United,Carlton Cole wamenusurika kwenda jela miaka mitano kila mmoja na faini ya Rupia Milioni 500 baada ya mamlaka za juu za Indonesia kuwakuta na hatia ya kukiuka sheria za uhamiaji za nchini humo. 

    Essien na Cole ambao wako nchini humo wakiwa ni wachezaji wapya wa klabu ya Persib Bandung inayoshiriki ligi kuu ya Indonesia,Jumamosi iliyopita walishuka dimbani kuichezea timu hiyo dhidi ya Arema FC wakiwa hawajakamilisha taratibu za uhamiaji.

    Katika utetezi wake uongozi wa Persib Bandung umesema uliamua kuwatumia wachezaji hao baada ya kupata baraka kutoka kwa chama cha soka cha nchi hiyo IFA.

    Katibu mkuu wa chama cha soka cha Indonesia IFA,Joko Driyono amekiri kuwa waliipa baraka zao Persib Bandung kuwatumia wachezaji hao kutokana na ukweli kwamba zoezi la upatikanaji wa vibali vya kazi nchini humo kuwa ni la taratibu sana.

    Wakati huohuo Maulia Purnamawati ambaye ni mkuu wa idara ya uhamiaji ya mji wa Bandung amesema ofisi yake imewasimamisha wachezaji hao kucheza mpaka hapo watakapokuwa wamekamilisha taratibu zote za masuala ya uhamiaji.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Michael Essien anusurika kwenda jela miaka mitano Indonesia. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top