Mwanza,Tanzania.
LIGI KUU ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) itaendelea tena leo Ijumaa kwa mchezo mmoja wa ligi hiyo kuchezwa huko jijini Mwanza kwenye dimba la uwanja wa CCM Kirumba ambapo Wanakishamapanda,Toto Africans watakuwa wenyeji wa Maafande wa JKT Ruvu kutoka Mlandizi,Pwani.
Timu hizo zinaingia kwenye mchezo wa leo zikisaka alama tatu muhimu ili kukwepa mkasi wa kushuka daraja.Toto Africans iko nafasi ya 14 ikiwa na alama 26 katika michezo 26.JKT Ruvu iko nafasi ya 16 ikiwa na alama 23 katika michezo 27.
0 comments:
Post a Comment